29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

DONDOO

REAL MADRID

BAADA ya klabu ya Real Ma dridkufanikiwa kutwaa Kombe la UEFA Super Cup dhidi ya Man United, Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuuza mshambuliaji wa pembeni, Gareth Bale, mchezaji huyo amehusishwa kutaka kujiunga na Man United.

Chelsea

MABINGWA wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, wametenga kiasi cha pauni milioni 25 ili kuinasa saini ya nyota wa klabu ya Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain. Mchezaji huyo ameweka wazi kuwa anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Inter Milan

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez, anaweza kuonekana msimu ujao akiwa amevaa jezi ya Inter Milan kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya kutaka kumsajili wakati huu wa majira ya joto.

Chelsea

KOCHA wa mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, Antonio Conte, ameweka wazi kuwa yupo kwenye mipango ya kutaka kuinasa saini ya nyota wa klabu ya Tottenham, Danny Rose, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wakati huu wa kiangazi.

PSG

MATAJIRI wa klabu ya PSG wanataka kuonesha tena jeuri ya fedha kwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez. PSG wamesema wametenga kiasi cha pauni milioni 80, ili kuinasa saini ya nyota huyo.

Barcelona

KLABU ya Barcelona, tayari imefikia makubaliano na nyota wa klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho. Mchezaji huyo amewaomba Liverpool wamruhusu kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto. Lakini kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, anaonekana kukataa kumuuza.

Valencia

KLABU ya Valencia, imesema ipo kwenye mipango ya kuwania saini ya beki wa klabu ya Arsenal, Gabriel Paulista. Klabu ya Arsenal imesema ipo tayari kumuuza mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 10. Wenger amedai mchezaji huyo hayupo kwenye mipango yake msimu ujao.

Chelsea

NYOTA wa klabu ya Leicester City, Danny Drinkwater, amesema yupo kwenye mipango ya kuzungumza na uongozi wa klabu hiyo juu ya kuondoka kwake. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea.

Chelsea

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, yupo kwenye mipango ya kutaka kuzungumza na beki wa pembeni wa klabu ya PSG, Serge Aurier. Kocha huyo amesema anataka kuimarisha kikosi chake ili kuweza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Real Madrid

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard, amewaomba mabingwa hao wa nchini England wamruhusu aondoke katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji. Nyota huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania, Real Madrid.

Man City

KOCHA wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, anatarajia kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Barcelona juu ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu hiyo, Sergio Busquets. Kocha huyo aliwahi kufanya kazi na Busquets ndani ya Barcelona.

PSG

KLABU ya PSG, inataka kuonesha jeuri ya fedha kwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Monaco, Kylian Mbappe, huku wakisema wanatenga pauni milioni 161 kuinasa saini yake. Wiki moja iliyopita walikamilisha usajili wa Neymar kwa uhamisho wa pauni milioni 198.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles