Snura: Sivai nguo za utupu tena

0
2058

snuraNA RHOBI CHACHA
MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Majanga’, amesema hatavaa nguo za nusu uchi tena kwa kuwa ameshagundua makosa hayo.
Snura alisema awali alikuwa akivaa mavazi ya nusu uchi au nguo za kumbana, lakini kwa sasa amejirekebisha na anatambua nguo zinazompendeza ili kutokuleta sintofahamu kwa mashabiki wake.
“Kiukweli nashukuru ushauri wa watu katika suala la mavazi, nimeshajirekebisha kwa sasa sivai kama zamani mavazi yasiyofaa katika jamii,” alieleza Snura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here