Riyama Ally: Najifunza kwa Thea

0
1475

RiyamaNA RHOBI CHACHA
STAA katika uigizaji, Riyama Ally, ameibuka na kudai kwamba vitu vingi vya uigizaji hujifunza kutoka kwa msanii mwenzake, Ndumbaro Misayo ‘Thea’.
Riyama alisema Thea ni msanii zaidi yake na huwa hajibweteki kwa kulewa sifa kama walivyo baadhi ya waigizaji, ndiyo maana hupenda kujifunza kwake.
“Mimi najiamini na huwa napenda kumpa pongezi mtu anayefanya vizuri katika sanaa, Thea tangu alivyoanza kuigiza hajawahi kutetereka kwa kuwa halewi sifa za mashabiki wake, hivyo ni mfano wa kuigwa na wasanii wengine,” alimaliza Riyama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here