27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ali Kiba, Diamond, Jux wapeta tuzo za Kili

Diamondalikiba1juxNA ZAITUNI KIBWANA
WASANII wa muziki wa bongo fleva, Ali Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Juma Jux, wameingia katika vinyang’anyiro sita vinavyogombewa katika tuzo za muziki ‘Kili Music Award’.
Ali Kiba ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume, mtunzi bora, video bora ya mwaka na mwimbaji bora wa Afro-Pop.
Naye Diamond ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora, mwimbaji bora, mtunzi bora, wimbo bora wa Zouk, wimbo bora wa Afro Pop na Video Bora ya mwaka kupitia wimbo wa ‘Nitampata Wapi’ na ‘Mdogo Mdogo’.
Pia Juma Jux naye ameingia kwenye kipengele cha mwimbaji bora wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume na wimbo bora wa R&B kupitia nyimbo zake mbili za ‘Sisikii’ na ‘Nitasubiri’.
Mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania Basata, Kurwijira Maregesi, alisema zoezi rasmi la upigwaji wa kura litaanza Mei 4 na kufungwa Juni 5 mwaka huu kwa udhamini mkubwa wa Kampuni ya TBL, kupitia bia yake ya Kilimanjaro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles