28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Natamani kikubwa zaidi ya ubingwa VPL

NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van Der Pluijm, amesema ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kitu kidogo sana kwake, kwani bado nafsi yake inatamani kitu kikubwa zaidi kwa klabu hiyo.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1dhidi ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi uliofanyika Jumatatu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kufikisha jumla ya pointi 53, zilizopelekea klabu hiyo kutangazwa kuwa mabingwa wapya msimu huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema tayari amejipatia sifa hapa nyumbani kwa kuipa ubingwa Yanga, akieleza sasa ni wakati wa kuonyesha maajabu kimataifa.
Pluijm alisema kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, tayari mikakati yake yote ambayo alijiwekea kabla ya mchezo huo wa marudiano imekamilika.
“Ubingwa wa ligi ni kitu kidogo kwangu, hapa kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuelekeza nguvu zote kimataifa,” alisema Pluijm.
Mholanzi huyo alisema wakati anakabidhiwa kikosi cha Yanga, alijiwekea dhamira ya kuwapa ubingwa na hilo limeweza kutimia.
“Nilipokuwa naingia mkataba nilisema lazima timu ninayoifundisha ichukue kombe la ligi, bado nataka kuishuhudia ikifanya kitu kikubwa zaidi,” alisema Pluijm.
Timu hiyo inatarajiwa kuvaana na Etoile du Sahel katika mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Tayari timu hiyo imetua Tunisia kwa ajili ya mchezo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles