24.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 17, 2021

Snura kuwapoza wenye migogoro ya ndoa

snura.jjpgNA THERESIA GASPER
MKALI wa wimbo wa ‘Majanga’, Snura Mushi, amesema kwa sasa ameelekeza kuwapa faraja wanawake wanaokumbwa na matatizo katika ndoa zao.
Snura aliyezindua wimbo wake mpya wa ‘Hawashi’ hivi karibuni mjini Songea, alisema wimbo huo umelenga kuwafuta machozi wanawake hao.
“Hawashi imeelezea matatizo wanayokutana nayo wanawake wenzangu katika maisha ya kila siku hasa pale wanapokuwa wameolewa, kama unavyojua visa vya wanaume lakini mbaya anaonekana mwanamke,” alisema Snura.
Wimbo huo umetayarishwa chini ya mtayarishaji, Mesen Selekta, huku akiwa ameshirikiana na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribariki ‘Ney wa Mitego’.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,986FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles