24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Busungu, Mandawa hao wakaribia Simba

simbaNa Judith Peter, Dar es Salaam
WASHAMBULIAJI wawili, Rashid Mandawa na Malimi Busungu, wanakaribia kutua ndani ya timu ya Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mandawa (Kagera Sugar) na Busungu (Mgambo JKT) ni moja ya washambuliaji wazawa waliofanya vizuri ligi kuu msimu uliopita, Mandawa akicheka na nyavu mara 10, huku straika mwenzake huyo akifunga nane.
Chanzo cha ndani ya Simba kililipasha MTANZANIA jana kuwa mazungumzo yao na wawili hao yamefikia sehemu nzuri na muda wowote dirisha likifunguliwa wanatarajia kuwasainisha mikataba.
“Kiufupi msimu ujao tunataka kuimarisha sehemu yetu ya ushambuliaji ambayo imeonekana kupwaya, Mandawa na Busungu ni moja ya wazawa waliofanya vizuri, hivyo tunataka kuhakikisha tunawanasa,” kilieleza chanzo hicho.
Kagera Sugar kupitia kwa Meneja wake, Mohamed Hussein, alisema jana kuwa hawawezi kumzuia mshambuliaji huyo kujiunga na Simba na timu nyingine yoyote inayomuhitaji.
“Sisi hatuna shida na mchezaji yeyote ambaye atatakiwa na klabu nyingine kama taratibu zitafuatwa kikamilifu hatuwezi kuwa na pingamizi kwani tunaamini wapo wachezaji wengi wazuri na wenye uwezo,” alisema.
Mbali na Mandawa kutakiwa na Simba, pia Meneja wake, Jamal Kisongo, anamfanyia mpango wa kwenda kufanya majaribio katika timu ya TP Mazembe (DRC) na hivi sasa anasubiri baraka za mmiliki wa timu hiyo, Moise Chapwe Katumbi.
Naye Busungu, akizungumza na gazeti hili jana alisema: “Sitaki kulizungumzia sana suala hilo, ila Simba ndio nipo kwenye mazungumzo nayo ya karibu na usiwe na haraka muda wowote nitakwambia naenda wapi.”
Simba inahaha kufanya marekebisho kwenye kikosi chake baada ya kushindwa kufuzu michuano ya Afrika ngazi ya klabu kwa mwaka wa tatu mfululizo, msimu ujao imepania kuchukua ubingwa mbele ya wapinzani wake Yanga na Azam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles