Nisha: Mashabiki acheni kuazima vya watu

0
1449

nishaaaNA MWALI IBRAHIM
MSANII wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amewataka mashabiki wake wenye tabia ya kuazima vitu kwa marafiki zao waache kwa kuwa vinaweza kuwaletea madhara makubwa.
Licha ya somo hilo kulitoa katika filamu yake ya ‘Mtaa kwa Mtaa’, pia ameweka wazi kwamba kuazima nguo ama vitu vingine kunaweza kumkosesha amani ama heshima mwazimaji jambo ambalo litampotezea muda wa kufanya maendeleo.
“Hilo ni moja ya somo kwenye filamu yangu hiyo, naamini wapo watakaojifunza kulingana na hilo, nimeuvaa uhusika huo ili kutoa somo hilo kwa mashabiki wangu,” alisema.
Filamu hiyo imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo mwanamama aliyejaa vituko, Asha Boko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here