22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Snoop Dogg afungua mtandao wa watumiaji bangi

snoop-624-1368121236NEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki nchini Marekani, Snoop Dogg, amefungua mtandao wake mpya ambao utawahusisha watu wanaotumia bangi na vitu vya asili hiyo.

Mtandao huo ameupa jina la ‘Merry Jane’, huku akiwataka wanaotaka kujua zaidi kuhusu bangi wajiunge nao kwa ajili ya kufahamu zaidi, kingine kilichopo katika mtandao huo ni habari za biashara, siasa, utamaduni na afya.

Snoop Dogg amesema mtandao huo utafunguliwa rasmi Oktoba mwaka huu na tayari amefanya mazungumzo na baadhi ya watu maarufu ambao wako tayari kuhudhuria kwenye ufunguzi huo.

“Kuna watu mbalimbali ambao wapo tayari kuungana na mimi katika zoezi hilo kama vile Seth Rogen na watu wengine mbalimbali, ninaamini siku zinavyozidi kutakuwa na ongezeko kubwa la wanachama,” alisema Snoop Dogg.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles