P-Square wawachefua mashabiki mtandaoni

0
893

psLAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambao wanaunda kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye, wamewaacha midomo wazi mashabiki baada ya kuweka picha ya uchi mtandaoni.

Inasemekana picha hiyo iliwekwa na Peter katika akaunti yake ya Instagram ambayo inamuonesha mwanamume akiwa uchi lakini sura yake haikujulikana.

Baadhi ya mashabiki wakiwa njia panda huku wakijiuliza picha hiyo ni wao wenyewe au mwanaume gani, pia wamelishangaa kundi hilo kwa tabia hiyo chafu.

Hata hivyo, Peter kupitia ukurasa wake huo aliomba radhi kwa kuiweka picha hiyo huku akidai alijisikia kuiweka picha hiyo lakini baada ya muda aliitoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here