Lollipop: Waumini hawasikilizi kinachoimbwa katika injili

0
699

photoNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa muziki wa Injili nchini, Goodluck Gozbert, maarufu kwa jina la Lollipop, amesema muziki wa injili una changamoto nyingi, ikiwemo ya mashabiki wake wengi kutofuata maneno yanayoimbwa katika nyimbo hizo.

Msanii huyo alisema waumini wanatakiwa kuanza kusikiliza na kufuata kinachoimbwa katika nyimbo hizo kwa kuwa zina ujumbe mwingi kwao, badala ya kucheza midundo huku wakiendelea kutenda mabaya.

“Ni utamaduni uliojengeka kwa muda mrefu tunafuata zaidi burudani iliyopo katika muziki ambayo inatokana na vinanda, gitaa na midundo yake katika muziki, lakini tunasahau kusikiliza kwa makini ujumbe muhimu uliopo katika nyimbo hizo,” alisema Lollipop.

Lollipop ambaye pia ni prodyuza anafanya vizuri katika muziki wa injili baada ya kuachia nyimbo mbili, ‘Ipo Siku’ na ‘Waambiane’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here