Lulu: Nampenda Wema kama dada yangu

0
1417

lulu_instagramNA THERESIA GASPER

KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepetu, utakuwa umekosea, kwani hakuna ugomvi kati yao.

Lulu alieleza kwamba wamekuwa wakishirikiana na Wema Sepetu katika mambo mbalimbali, ikiwemo sherehe, misiba na mijumuiko mbalimbali.

“Nampenda Wema kama dada yangu na yeye ananipenda vile vile, nimekuwa nikihudhuria kwenye shughuli mbali mbali ambazo zinamhusu, nilishiriki vema katika msiba wa baba yake na sherehe zake mbalimbali,” alisema.

Lulu na Wema ni wasanii waliokumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya sanaa, lakini wameweza kuendeleza umaarufu wao hadi sasa na wamejizolea idadi kubwa ya mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here