Nay wa Mitego: Wasanii tusiwe wanasiasa

0
1123

nayNA ESTHER MNYIKA

MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Emanuel Eribarik ‘Ney wa Mitego’ amewataka wasanii wenzake wawe wahamasishaji wa wananchi ili kujitokeza na kupiga kura Oktoba 25, badala ya wao kugeuka kama wanasiasa wanaogombea katika siasa.

Ney wa Mitego aliandika katika ukurasa wake wa ‘Instagram’ kwamba wasanii wamejisahau, wamekuwa wanasiasa na wagombea, jambo litakalokuja kuwagharimu baada ya uchaguzi huo.

“Wasanii tubaki kuwa wahamasishaji tu, kuanza kukashifu viongozi utadhani nasi wanasiasa au wagombea wa nafasi mbalimbali za kisiasa si jambo jema kwa maisha ya muziki wetu baada ya Oktoba 25.

“Wakati mwingine huwa najiuliza wanalipwa kiasi gani, maana wanasahau kwamba wana mashabiki wenye itikadi tofauti kisiasa na kuna maisha baada ya uchaguzi,’’ alieleza Nay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here