27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

SMG amkumbusha wajibu Eymael

Zainab Iddy, Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa timu ya vijana ya Yanga, Said Maulid ‘SMG’, amemuomba kocha wa kikosi cha wakubwa cha timu, Luc Eymael, kutenga muda kwa ajili ya kukitembelea kikosi chake.

 SMG ambaye aliwahi kuwa nyota wa Yanga kabla ya kustaafu na kugeukia ukocha, aliliambia MTANZANIA jana kuwa , tangu Eymael akabidhiwe kikosi cha wakubwa cha Yanga, hajawahi kutembelea mazoezi ya vijana wake zaidi ya kukutana nao katika mechi za utangulizi za Ligi Kuu.

“Niwe mkweli, kocha Eymael hajawahi kuja mazoezini kutembelea wala kuzungumza na wachezaji, naomba nichukue nafasi hii kumuomba siku moja atenge muda wa kufanya hivyo ili kuongeza hali ya kujituma kwa vijana.

“Alishakuja kuonana na wachezaji mara moja au mbili baada ya kucheza mechi za utangulizi za Ligi Kuu, baada ya kuwaona wakicheza alikuja kuwaambia kuwa bado kuna vitu havipo sawa kwenye timu lakini hakuweka wazi,”alisema.

Alisema mazingira ya aina hiyo yanaweza kuwakatisha tamaa makinda hao kwakua wanaweza kuingiwa na fikra kwamba hawana nafasi ndani ya Yanga.

“Suala la kocha wa timu kubwa kuwaona vijana ni sehemu ya kikosi chake, ilikuwa ikifanywa na Hans Van der Pluijm na Mwinyi Zahera, tangu hapo hakuna anayefuatilia timu hii,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles