27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Azam,Namungo waingilia dili la Yanga

Zzainab Iddy, Dar es salaam

KLABU za Azam na Namungo, zinafukuzia sanini ya kiungo Cleophance Mkandala, anayekipiga ndani ya kikosi cha Tanzania Prisons, anayewaniwa pia na Yanga.

Yanga ndio ya kwanza kuitaka saini ya kiungo huyo, ikilenga kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mkandala ameonekana kuzigonganisha timu hizo, baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu, ambapo ameweza kutoa pasi nne zilizozaa mabao ya Prisons na kufunga mawilihivyo kuisaidia kupatikana kwa mabao sita kati ya mabao 27, yaliyofungwa maafande hao kwenye mechi 28 walizoshuka dimbani.

Taarifa ambazo MTANZANIA ilizozipata kutoka ndani ya Azam FC,zinasema kuwa, Azam inamuhitaji mchezaji huyo baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo ya Chamazi pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, Arstica Cioaba kujumuisha jina lake katika orodha ya nyota wapya anaowahitaji.

“Jina hilo lipo katika orodha ya wachezaji wapya wanaotakiwa na timu yetu, lakini bado hatujafanya mazungumzo nae kwa sababu tunakamilisha mikataba ya wachezaji wa ndani wanaomaliza muda wao,”alisema mtoa habari huyo.

Wakati Azam ikivuta pumzi, Namungo nao wameonekana kumtolea macho baada ya Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hassan Zidadu kuweka wazi kuwa ni mchezaji mzuri na kama watafanikiwa kumpata litakuwa jambo la faraja kwao.

“Mkandala ni kijana mdogo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza soka, Namungo tunataka watu wa aina hiyo,ikitokea tukampata utakuwa sajili bora kwetu,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles