25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sitta aongoza kuaga mwili wa Kihwele

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta jana ameongoza wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Erasto Kihwele aliyefariki dunia Aprili 17 mwaka huu.
Marehemu Kihwele aliagwa na mamia ya watu katika ukumbi wa TAZARA ambako huzuni na vilio vilitawala.
Akizungumza wa kutoa salamu za rambirambi,Waziri Sitta alisema alimfahamu Kihwele muda mfupi.
Alisema enzi za uhai wake, alibaini kuwa alikuwa mpiganaji wa haki za wanyonge nafasi ambayo ina watu wachache nchini, ikizingatiwa wengine wakishika nafasi kama hiyo wanaiba.
“Wapiganaji ni wachachewengi ni wadokozi, wahujumu na wezi, kusingekuwa na maombi taifa lingekwisha.
“Erasto ametutoka,kuna vitu ametuachia kama vile kuhakikisha wafanyakazi Tanzania hawanyanyaswi,wizi mkubwa haufanyiki, wapiganaji tupo tutaendelea kupigana, yote uliyoniambia ofisini tutayafuatilia,”alisema.
Aliwaasa wengine waendelee kudai haki badala ya ubinafsi na kwamba wale wezi wote ufike wakati wafungwe katika magereza ya Ukonga au Segerea.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa TRAWU, Boaz Nyakeke alisema Kihwele alichaguliwa kushika wadhifa Katibu Mkuu wa TRAWU Septemba 8, 2011.
Alisema alikitumikia chama hicho kwa miaka mitatu hadi alipoanza kuugua Machi mwaka huu.
Alisema marehemu alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Aprili 13 mwaka huu aliruhusiwa. Ilipofika Aprili 15 mwaka huu hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na akapelekwa Hospitali ya Kairuki Mikocheni ambako Aprili 17 mwaka huu alifariki dunia.
“Wakati wa uhai wake, Kihwele alipigania kupata ufumbuzi wa matatizo ya mishahara kwa wafanyakazi, alidai nyongeza za mishahara na alikemea ubadhirifu katika Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) yaliponunuliwa mabehewa mabovu kutoka India.
“Kaondoka shujaaa, mtetezi wa haki za wafanyakazi,tutaendelea kumkumbuka kwa kupiga vita ufisadi na ubadhirifu,”alisema.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafannyakazi Tanzania (TUCTA), Nicolas Mgaya alisema miaka michache iliyopita mwezi kama huu,Katibu mwingine wa TRAWU,Silvesta Rwegasira alifariki dunia.
Mwenyekiti wa TRAWU, Mussa Kalala alisema mwili wa marehemu Erasto utazikwa kijijini kwao Kihese mkoani Iringa baada ya taratibu zote kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles