30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

20 Chadema wajitokeza Segerea kuwania ubunge

Dk. Makongoro MahangaNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
MAKADA 20 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema) wameonyesha nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Segerea.
Mbali ya makada hao, watu wengine 50 wamejitokeza kuwania nafasi ya udiwani katika jimbo hilo.
Kwa sasa mbunge wa jimbo hilo ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga aliyeshinda katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kura 43,554 (asilimia 41.7) wakati mpinzani wake,Fred Mpendazoe (Chadema) alipata kura 39,150 (asilimia 37.49).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea, Gango Kidero alisema lengo ni kutetea maslahi ya wananchi ndani ya jimbo hilo.
Alisema licha ya makada hao kuonyesha nia,uamuzi wa mwisho upo kwa viongozi wa juu wa chama hicho kupitisha jina la mgombea mmoja baada ya Chadema kuungana na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa).
“Tuna zaidi ya watu 70 walioonyesha nia ya kuwania ubunge na udiwani wa Jimbo la Segerea lengo ni kulichukua kutoka mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi(CCM),”alisema Kidero.
Alisema watangaza nia wote ni wasomi wazuri wenye fani mbalimbali na wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi ndani na nje ya jimbo hilo.
Alisema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana,Chadema kilipata viti 16l ambavyo ni asilimia 26 na wajumbe 56.
Matokeo hayo ni tofauti na mwaka 2009 ambako chama hicho kilipata kiti kimoja, alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles