26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SITA WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO DAR

Na LEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

WATU sita, akiwamo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi, ambaye ni Imamu wa Msikiti wa Huda Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni baada ya kukamatwa na meno 28 ya tembo, yenye uzito wa kilogramu 377.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 13 na 14, mwaka huu, huko Mbezi Beach, wakiwa wameyahifadhi meno hayo kwenye ghala.

Waziri Maghembe alimtaja mwenyekiti huyo kuwa ni Bakari Seruni, wengine ni Mohamed Yahaya, Juma Jebo, Hamisi Omari, wote wakazi wa Dar es Salaam, Amiri Shelukindo, mkazi wa Gairo, mkoani Morogoro na Ahmed Bakari, mkazi wa Mkuranga, Pwani.

Alisema kati ya meno hayo, 21 yalikutwa yamefichwa kwenye ghala, mengine  saba yalikuwa yamehifadhiwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao.

“Jana usiku mmoja wao alituambia tusimsumbue mke wake ili tumwambie atuonyeshe meno ambayo yamefichwa ndani, ndiyo tukafanikiwa kuyakamata hayo meno saba.

“Wataalamu wameyapima meno haya yanaonesha hawa tembo wameuawa kama miaka mitatu iliyopita, kwa hiyo inaonesha kuwa waliua tembo wengi wakatunza mzigo nyumbani, sasa wanatafuta wanunuzi,” alisema Profesa Maghembe.

Aliwataka wale wanaojihusisha na uwindaji haramu, ikiwamo wa tembo na faru kuachana na kazi hiyo na kufikiria kazi nyingine, kwani kuendelea na kazi hiyo kutawafanya kwenda jela kwa miaka isiyopungua 25.

Aliongeza kwamba, pamnoja na China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo, bado biashara hiyo inashamiri katika mitandao mbalimbali, hali inayochangia kukwamisha mapambano dhidi ya ujangili wa tembo na ndovu katika maeneo mbalimbali duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles