21.4 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Siri yavuja mastaa Bongo Muvi kula bata Zanzibar

SWAGGAZ RIPOTA

MAMBO yameendelea kunyooka kunako tasnia ya filamu. Unaambiwa sasa hivi wasanii wa Bongo Muvi wanakula bata kama lote katika visiwa vya Zanzibar, huku wakipanga mipango ya kunufaika zaidi  na kazi zao.

Bata la wasanii hao lilianza mwanzoni mwa wiki hii, ambapo walichukua ndege binafsi kutoka Dar es Salaam na kupaa mpaka kwenye fukwe za Michamvi na Paje huko Zanzibar kufanya mapumziko ikiwa ni muda mfupi bada ya kuingia makubaliano na kampuni ya SwahiliFlix.

Ray Kigosi na Chuchu Hnsy wakiwa Zanzibar

Kampuni hiyo ambayo imeingia kwa kasi kwenye tasnia ikiwa na lengo la kuwanufaisha zaidi ya wasanii na kuwapa burudani mashabiki wa filamu za Kiswahili, inatarajia kuzinduliwa rasmi  Julai 31 mwaka huu katika ukumbi wa  Mlimani City.

Swaggaz, limedokezwa kuwa katika uzinduzi wa SwahiliFlix,  kutoka unyamwezini atadondoka staa wa filamu duniani, Will Smith na mrembo Genevieve Nnaji wa Nigeria lengo likiwa ni kuipa hadhi na heshima tasnia ya filamu Bongo katika anga la Kimataifa.

SwahliFlix, yenye jumla ya filamu 1,000 za Kiswahili,  ina wigo mpana wa kuwafikia mamilioni ya mashabiki duniani kote kwa njia rahisi kupitia simu ya mkononi, kompyuta, iPad na vifa vingine kama hivyo.

Dude kushoto akiwa na Chuchu Hansy Zanzibar

Ambapo, shabiki hulipia fedha kulingana na kfurushi anachotaka, anaweza kulipia wiki, mwezi, miezi au mwaka na akawa anatazama (Stream), kupatua (download) filamu zote za Kiswahili ambazo zinapatikana katika mtandao huo.

Ili kufanikisha mchongo huo  asilimia kubwa ya waigizaji wamedondosha wino katika mikataba ya kufanya kazi na SwahiliFlix na kwa kuanzia kampuni hiyo, imeanza kuwapa bata la nguvu mastaa kadhaa ambao ni mabalozi wao.

Nazir, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa SwahiliFlix, ameling’ata sikio Swaggaz siri ya bata la wasanii hao visiwani Zanzibar kwa kusema :“ Kilichotuleta Zanzibar ni kupanga  sherehe nzima ya uzinduzi tarehe 31, utakuwa vipi, ndiyo maana hii kamati imewekwa huku, tunapanga mambo mengi siku hiyo itakuwa vipi ila tofauti na hapo kuna ajenda zetu tofauti kwa mfano, kunatengeneza maudhui zaidi, kufanya video za hapa na pale kwaajili ya promo y App yetu mpya IoS, Android, tovuti yetu na Instagram yetu na Irene Uwoya ndiyo mkuu wa kamati ya upangaji, anakuwa anatupa maendeleo ya mipango yetu.”

Johari, JB na Ben Kinyaiya

Naye Irene Uwoya ambaye wiki hii amekuwa gumzo baada ya watu kuhangaika kuitafuta video ya ngono inayodaiwa kuwa ni yake amesema : “Huu ni muda wa mapinduzi kwenye tasnia ya filamu, tumesemwa sana lakini sasa hivi tumeamua kufanya kweli kwa sababu SwahiliFlix inaenda kukomboa tasnia ya filamu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles