Anna Potinus – Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amevitaka vyama vya siasa nchini kujenga utaratibu wa kujifunza miongoni mwao ili kuendeleza amani ya nchi ambapo amviatka vyama hivyo kufanya jambo hilo kwa unyenyekevu.
Ametoa rai hiyo leo Jumamosi, Julai 27, alipokuwa akizungumza katika mkutani wa chama cha NCCR Mageuzi wa kuchagua viongozi wapya wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dae rs Salaam.
“Ninashukuru leo mmepata nafasi ya kutuita hapa na ninawaombea muendelee hivyo, Mbatia huwa ninakuangalia huwa unasema mambo mengi ya busara hivyo ongoza chama hiki kiwe cha busara na kisaidiane na chama tawala nacho kijifunze,” amesema.
“Mimi ninajifunza kwenu miaka yangu 81 ninawafundisha na kujifunza pia, ninyi vyama mlivyotangulia na vilivyozaliwa jengeni uwezo kwa kujifunza miongoni mwenu, CCM mjifunze kwa vingine na ninyi mjifunze kutoka kwao pia na mfanye hivyo kwa unyenyekevu,” amesema.
Aidha amesisitiza vijana kuwa na utu kwakua ndio msingi wa Taifa la Tanzania ambapo amesema iwapo kutakuwa na utu, usawa na na haki nchi itakuwa na amani.
“Ninawakumbusha vijana taifa hili wakati linaasisiwa msingi wake ulikua ni utu na usawa wa utu ukikataa hilo maana yake unakataa utu kwasababu mwenzako nae anaweza akakukataa,” amesema.
“Usawa na utu hautoshi lazima kuwe na haki maana kila mtu anastahili haki, msingi huo ndio unatawala vyama vyetu vyote hivyo tukifanya hayo tutapata amani,” amesema.