26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Singida yavuka lengo ukusanyaji mapato

NA SEIF TAKAZA, SINGIDA

Mkoa wa Singida umevuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka asilimia 90 hadi asilimia 101 kwa kukusanya bilioni 21.32 kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Akizungumza wakati wan kufungua kikao cha ushauri cha Mkoa jana, kilichofanyika katik

a ukumbi wa RC Mission mjini hapa, Mkuu wa mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema, malengo hayo yamefikiwa kutokana na mikakati mathubuti, ikiwemo uanzishwaji wa vyanzo vipya vya mapato na utendaji mzuri wa wanaohusika kukusanya.

“Nawapongeza kwa hatua hizi mlizochukua kwa kuvuka malengo katika ukusanyaji wa mapato ongezeni bidii zaidi katika ukusanyaji, Amesisitiza Dendego.

Dendego pia amezipongeza Halmashauri za mkoa wa Singida kwa kupata hati safi katika ukaguzi.

Kuhusu fedha za Miradi ya Maendeleo, Mkuu huyo wa mkoa, ameishukuru Serikali kwa kuupatia Mkoa wa Singida bilioni 241 sawa na asilimia 105 kwa ajili ya shughuli za utawala na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amevunja rekodi ya kuupatia mkoa wa Singida fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikilinganishwa na miaka mingine ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 mkoa uliidhinishiwa zaidi ya bilioni 230 lakini umepewa fedha zaidi ya bilioni 241 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Sijawahi kuona katika miaka yangu ya Uongozi kwa Serikali kutoa fedha zaidi ya tulizoomba lakini kwa Rais Samia hili limewezekana tunamshukuru sana tena sana,” amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.

Kuhusu miradi ya umwagiliaji, amesema Serikali inaendelea kukarabati na kujenga miradi mipya ya umwagiliaji ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Amesema kwa sasa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umwagiliaji inaendelea vizuri ukiwemo mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkalama na Msange katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 55.

Dendego ameeleza kuwa miradi hiyo miwili ya umwagiliaji ikikamilika itaufanya mkoa huo kuwa na hekta 4000 za umwagiliaji hali ambayo itaongeza maradufu shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles