27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SIMU ZA MKONONI ZILIVYOUA MAWASILIANO YA BARUA

 

 

Na Mwandishi Wetu,

MOJA ya mambo muhimu ambayo katika ulimwengu wa sasa wa mawasiliano, hayakwepeki ni pamoja na matumizi ya simu za mkononi. Matumizi ya simu za mkononi yamerahisisha mambo mengi kutokana na teknolojia yake kukua kwa kasi kila kukicha.

Kwa mfano, katika robo ya eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, watu wanaweza kuwasiliana kwa kupigiana simu, kuandikiana ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha kama vile Tigopesa na huduma nyingine ikiwamo intaneti.

Takwimu zinaonesha kuwa utaratibu wa kujuliana hali kwa kuandika barua umepungua kwa kiasi kikubwa na wataalamu wanadai kuwa huenda ukakoma kabisa kwa mtu mmoja mmoja na kubakia katika mawasiliano ya kiserikali na kampuni ambazo wakati mwingine hulazimika kufanya hivyo.

Ongezeka la uwapo wa aina tofauti katika matumizi ya simu, ni changamoto kwa kampuni za simu, ili kubuni njia mbadala ambazo kwa kiasi kikubwa zitawahamasisha watumiaji wa simu kukubali bila kipingamizi kutumia huduma hizo ambazo kwa wakati mwingine zinawaingiza katika gharama za ziada.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa ukuaji uchumi uliofanywa na Benki ya Dunia (WB) mwaka 2009, katika nchi zinazoendelea ambako kuna uwezekano wa kutumia mtandao wa
inteneti, imeonekana kwamba ukuaji wa uchumi uliweza kufikia asilimia 1.4 kwa mwaka.

Kabla ya hapo, kulikuwa na watu takribani watano katika kila 100 ambao walimudu kutumia simu zao za mkononi kupata huduma ya intaneti.

Leo hii kuna mabadiliko makubwa ikilinganishwa na wakati huo.

Kila kampuni ya simu inajitahidi kubuni mbinu ambazo zitaisaidia kukaa na wateja wake na hata kupata wateja wapya. Mbinu hizi ni za aina tofauti, lakini kubwa zaidi ikiwa ni utaratibu wa kupandikiza ofa mpya kwa wateja kila kukicha.

Hivi karibuni, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo ilizindua ofa mpya kwa wateja wake, inayoitwa JazaUjazwe. Ofa hii inampa fursa mteja kuzawadiwa kutokana na kile atakachokuwa amenunua kwenda kwenye simu yake.

Anaweza kununua  miito ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno wakati anapojaza muda wa maongezi, iwe ni kupitia vocha ya kukwangua au Tigopesa.

Hapo ndipo ataongezewa kifurushi cha bure kwa huduma ile aliyonunua.

Kwa mujibu wa Tigo, kampeni ya JazaUjazwe imekuja kama  shukrani kwa wateja wa kampuni hiyo ya simu kutokana na uaminifu wao mkubwa kwa chapa hiyo.

Lakini pia kumekuwa na zawadi mbalimbali za ziada kupitia katika vipindi mbalimbali vya redio, iwapo mtumiaji atatoa ushuhuda wa kitu gani alifaidika nacho zaidi baada ya kupata ofa husika.

Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga anasema Tigo inathamini kuungwa mkono  ambako kumeoneshwa na wateja wake kwa kipindi cha miaka mingi, ndio maana wameona kuwa wateja wake wanastahili kupewa shukrani kwa imani
yao na kampuni hiyo.

Huu ni mfano mdogo wa Tigo, lakini bado kuna kampuni nyingine ambazo kwa namna ya pekee pia zinatoa ofa mbalimbali kwa wateja wake.

Baadhi ya wadau wa mawasiliano wanakwenda mbali zaidi na kuzitaka kampuni za simu kuja na ofa tofauti, ili kutoa fursa kwa watumiaji kupata unafuu wa matumizi ya huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni husika.

“Ofa hizi zipo, lakini kuna wakati kampuni hizi za simu zinafanya mchezo wa kuigana. Mwenzake akitoa ofa fulani, mwingine anatoa kama hiyo hiyo na kubadili jina kidogo, hili ni suala ambalo kampuni hizo zinatakiwa kulifanyia kazi.

“Ni dhahiri kuwa teknolojia ya simu za mkononi inashika kasi, kwa hiyo na ubunifu wa ofa na huduma nyingine unatakiwa zaidi,” anasema Victor Masato ambaye amekuwa wakala wa huduma za simu za mkononi kwa muda mrefu akitoa huduma za mitandao yote jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles