31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene akabidhiwa Jedwali la uchambuzi wa Sheria

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amepokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Bunge wa Saba kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ramadhani Suleiman.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Ramadhani Suleiman (katikati) akifafanua jambo.

Akizungumza wakati wa kupokea Jedwali hilo Septemba 2, 2022 Waziri Simbachawene amesema Serikali inaongozwa na sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaweza kutatua changamoto zote zinazogusa watu katika maswala ya sheria; kanuni, taratibu, mila na desturi zinazoongoza Serikali, alisema Waziri Simbachawene,” amesema Simbachawene.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Ramadhani Suleiman amemshukuru Waziri wSimbachawene kwa kupokea Jedwali hilo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba pamoja  na majibu aliyoyatoa kwa Kamati ya Bunge.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene (kushoto) akipokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge.
Judith Kapinga akifafanua jambo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo ilipokabidhi Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles