27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA YATUA 16 BORA SHIRIKISHO

Asha Kigundula -Dar es Salaam

TIMU ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho marufu Kombe la Azam (ASFC), baada ya jana kuichapa Mwadui mabao 2-1, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao yaliyoipa Simba ushindi yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 45 na Francis Kahata dakika ya 85, huku bao la Mwadui likifungwa na Mathias Gerald dakika ya 34.

Bao alilofunga Gerald jana linakuwa la pili kuitungua Simba, baada ya kuiliza pia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania msimu uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kumalizika kwa Mwadui kuvuna ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikionekana kuwa makini kujenga mashambulizi yake kuanzia nyuma kwenda katika lango la mpinzani.

Dakika ya tatu, Kahata  alishindwa kutumia vema nafasi aliyopata kuindikia Simba bao la kuongoza, baada ya kupokea pasi ya Chama lakini akiwa anatazamana na kipa wa Mwadui, Musa Mbisa, alifyatua mkwaju uliotoka nje.

Dakika ya sita, Omar Daga wa Mwadui alipoteza nafasi ya kuifungia timu yake bao la kuongoza, baada ya kushindwa kumalizia krosi iliyochongwa na Benjamini Sowah.

Dakika 21, Hassan Dilunga alipokea pasi safi ya Kagere lakini akaachiafataki iliyopaa juu ya lango la Mwadui.

Dakika ya 30, Sharaf Eldin Shiboub alikosa bao la wazi,  baada ya kutanguliziwa pasi ndefu na Chama na kuachia mkwaju ulipaa.

Dakika ya 34, Gerald aliindikia Mwadui bao la kwanza, akimalizia pande la Ludovick Evans.

Dakika ya 45, Chama aliisawazishia Simba kwa shuti kali la mguu wa kushoto, baada ya kuwazidi kasi mabeki wa Mwadui.

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kuja kivingine kwa lengo la kusaka ushindi.

Dakika ya 59, Kocha wa Mwadui , Khalid Adam alifanya mabadiliko alimtoa Gerald na kumwingiza Abdul Maskini.

Dakika ya79, Dilunga alilimwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Halfan Mbaruku wa Mwadui.

Dakika ya 80, Mwadui ilifanya mabadiliko mengine, alitoka Benjamini Saowah na nafasi yake kuchukuliwa na Maliki Jafar.

Dakika ya 85, Kahata aliindikia Simba bao la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Ibrahim Ajib.

Dakika ya 90, Simba ilifanya mabadiliko, alimtoa Mohammed Hussein ‘Tshabalala na kumwingiza Gadiel Michael.

Dakika 90 za mtanange huo zilikamilika kwa Simba kutakata kwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui.

Wakati Simba ilifuzu 16 bora, wapinzani wao Yanga watakuwa na kibarua cha kusaka tiketi hiyo watakapoikabili Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani hapo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitwanga Prisons bao 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Desemba 27,Uwanja wa Samora, Iringa.

Hata hivyo, leo Yanga itakuwa chini ya Kocha Mkuu mpya, Luc Eymael ambaye alirithi mikoba ya mtangulizi wake Mwinyi Zahera aliyefurushwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Wakati Yanga inaiadhibu Prisons Uwanja wa Samora ilikuwa inafundishwa aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu, Charles Mkwasa ambaye kwa sasa anamsaidia Eymael  katika benchi la ufundi. Wageni wao, Prisons wataingia na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wao uliopita wa ligi hiyo kwa Namungo kwa kuchapwa mabao 3-2, Uwanja wa Samora, Iringa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles