26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yapeta Kombe la FA

lyangaNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Simba jana ilifanikiwa kuingia kwa kishindo hatua ya nane bora ya michuano ya Kombe la FA baada ya kuichapa Singida United mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilikata tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Burkina Faso ya Morogoro mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Simba walioingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-3-3 kwa lengo la kuwashambulia zaidi wapinzani wao, waliandika bao la kuongoza dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji Danny Lyanga aliyeunganisha vyema pasi ya Emery Nimuboma.

Bao hilo liliwazindua Singida United na kujaribu kufanya mashambulizi langoni kwa Simba lakini hayakuzaa matunda.

Wakati Singida United wakijipanga, walijikuta wakifungwa bao la pili dakika 19 na mshambuliaji Hamis Kiiza aliyefanya shambulizi la kushtukiza na kupiga shuti la mbali lililojaa moja kwa moja wavuni.

Simba waliendelea kufanya mashambulizi langoni kwa Singida United ambapo dakika ya 21, Jonas Mkude alikosa bao la wazi huku Majwega akishindwa kufunga dakika ya 37 na 43.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Kiiza alifanikiwa kufunga bao la tatu dakika ya 68, kabla ya kocha Jackson Mayanja wa Simba kufanya mabadiliko ya kumtoa Lyanga nafasi yake kuchukuliwa na Said Ndemla.

Dakika ya 81, Awadhi Juma aliifungia Simba bao la nne baada ya kuunganisha pasi safi ya Namuboma na dakika ya 84 alihitimisha kwa kufunga bao la tano.

Dakika ya 90 Singida United walizinduka na kufunga bao la kusawazisha kupitia kwa Paulo Malamala aliyewapiga chenga Namuboma na kipa Vicent Agban na kujaza mpira wavuni.

Wakati huo huo Azam fc inatarajiwa kushuka dimbani leo katika uwanja wa ushirika, Mjini Moshi kuvaana na panone FC katika mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la FA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles