25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Tuliandaa mipango ya ushindi

plujimNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema ushindi waliopata juzi dhidi ya Cercle de Joachim ulikuwa ni moja ya lengo walilojiwekea kuhakikisha wanatinga raundi ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Yanga ambao waliwafunga Cercle de Joachim bao 1-0 ugenini wiki mbili zilizopita, juzi waliendeleza ubabe kwa wapinzani wao hao kwa kuwachapa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Mauritius wiki mbili zilizopita, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0, ambapo wamefanikiwa kusonga mbele wakiwa na jumla ya mabao 3-0.

Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya mchezo huo, Pluijm alisema matokeo ya ushindi yamezidi kuwapa wachezaji morali ya kuendelea kufanya vizuri katika raundi ya kwanza ambayo watakutana na APR ya Rwanda.

“Tumefurahi kuanza vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika, tumefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 na kufanikisha mipango tuliyojiwekea, sasa tunajiandaa kwa mchezo unaofuata dhidi ya APR,” alisema.

Alisema pamoja na ushindi waliopata, wachezaji wake walishindwa kuzitumia vyema nafasi nyingi walizopata kufunga mabao mengi, huku akiahidi kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili yasijirudie katika michezo inayofuata.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, alisema wanaendelea kujinoa kujiandaa na michezo mingine ili kupata matokeo mazuri zaidi, huku wakielekeza nguvu zaidi katika pambano dhidi ya Azam FC.

Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa wanaanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam uliopangwa kufanyika Machi 5, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga walitakiwa kucheza na Mtibwa Sugar kesho lakini wameomba mchezo huo usogezwe mbele hadi Machi 30, mwaka huu kupisha maandalizi ya kuwavaa wapinzani wao Azam na APR ya Rwanda katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Yanga wanaongoza katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 46 sawa na Azam waliopo nafasi ya pili kwa tofauti ya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles