24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Simba ‘yamchoka’ Jerry Muro

muroNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Simba umeliomba kwa mara nyingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumchukulia hatua za kisheria Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, kutokana na kauli zake mbaya na wasipofanya hivyo watamshughulikia wenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Simba, Haji Manara, alisema uongozi huo umechoshwa na kauli za kejeli, dharau, matusi yanayotolewa na Muro, akidai yamekuwa yakiwaathiri viongozi wa klabu hiyo.

Manara alisema, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita na timu yao kuambulia kipigo cha bao 2-0, Muro amekuwa akizungumza vitu vinavyoweza kuchochea vurugu kati ya klabu hizo mbili.

“Tumelazimika kusema kuwa tutamchukulia hatua Muro, maana TFF wamekuwa wakisikia maneno anayoyasema, lakini chakushangaza hakuna hatua yoyote wanayomchukulia, tunaomba waliangalie hili kabla yetu.

“Hii ni mara ya pili Muro kutukosea, mwaka jana alinikashifu mimi binafsi na tulipeleka malalamiko TFF ila hakuna maamuzi yoyote yaliyotolewa, badala yake walisema tusubiri Januari mwaka huu, lakini hadi sasa wameendelea kukaa kimya.

“Mimi binafsi nafahamu lugha chafu, hata viongozi wangu wanafahamu pia, lakini hatuna muda wa kuzitumia na tukisema tufanye hivyo, lazima TFF watatuchukulia hatua, sasa mbona wanashindwa kumuadhibu Muro,” alihoji Manara.

Manara alisema kukaa kimya kwa viongozi wa TFF, kunaonyesha wazi kuwa Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo imeshindwa kutimiza majukumu yake.

“Mpira siyo uadui, ni mchezo unaojenga amani na upendo, sasa nadhani Muro anataka kuleta chuki kati ya mashabiki, viongozi wa klabu hizi mbili,” aliongeza Manara.

Moja ya kauli za kejeli anazotumia Muro kwa wapinzani wao, ni kuifananisha Simba na timu zinazoshiriki ligi ya mchangani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles