27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Kaseja apata watoto mapacha

kasejaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

GOLIKIPA wa  zamani wa Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu kongwe nchini, Simba na Yanga, Juma Kaseja, anayekipiga Mbeya City, amefanikiwa kupata watoto mapacha, baada ya mke wake, Nasra Nassor kujifungua juzi mchana.

Kaseja amepata watoto mapacha wa jinsia ya kike na kiume, akiwapa majina ya Iqra na Iqram.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaseja alisema anamshukuru sana Mungu kwa kumletea zawadi hiyo maishani mwake, huku akiweka wazi kuwa imempa furaha sana.

“Nina furaha sana kupata watoto, nashukuru Mungu ndio mtoaji wa kila kitu na anampa atakae kwa muda anaotaka yeye,” alisema Kaseja, aliyeonekana ana furaha.

Kutokana na taarifa hiyo ya heri kufika kwa watu mbalimbali, baadhi ya wachezaji waliandika ujumbe kumpongeza Kaseja, wengi wao ni wale waliosoma naye Shule ya Sekondari Makongo ambao wameunda umoja unaojulikana kama Makongo All Stars (MAS).

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete, aliandika kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram na ule wa Whatsapp wa MAS kuwa, “Hongera mkwe kwa kuleta ‘twins’, sema nishaleta advance ya mahari kwako kwa ajili ya mke wangu.”

Kaseja alifunga ndoa na Nasra mwaka 2008 na wameishi pamoja kwa miaka yote hadi juzi walipofanikiwa kupata watoto hao mapacha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles