23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yajipanga kuitega TFF

Haji ManaraNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umepanga kulitega Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutoa msimamo wao kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba imetoa kauli hiyo baada ya TFF kuikubalia Azam FC kusogeza mbele mechi zake za Ligi Kuu, ili iweze kushiriki mashindano maalumu nchini Zambia, huku Yanga nao wakisuka mpango wa kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Yanga bado hawajawasilisha barua TFF ya kuomba kusogezwa mbele kwa mechi zake na kudai kuwa kama watafuata utaratibu huo shirikisho hilo litatoa uamuzi kwa kuangalia umuhimu wa ombi lao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema klabu hiyo itatoa msimamo wake leo baada ya Kamati ya Utendaji kukutana jana na kujadili mwenendo wa ligi na sitofahamu zinazoendelea.

“Tunashindwa kuelewa ligi inavyoendeshwa kienyeji, ndiyo maana uongozi umepanga kukutana leo (jana) jioni, ili tuweze kuweka wazi msimamo wetu,” alisema.

Azam iliomba TFF isogeze mbele mechi zake mbili za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons na Stand United, ili iweze kushiriki mashindano maalumu nchini Zambia yanayotarajia kuanza leo.

Katika hatua nyingine, Manara alisema kuwa klabu hiyo imeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja wake maeneo ya Bunju, ambapo wataalamu tayari wamechukua vipimo kwa hatua za awali.

“Ujenzi wa uwanja utaanza muda si mrefu, wataalamu tayari wameanza kufanya vipimo katika hatua za awali,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles