25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaifuata Plateau na ‘silaha’ 24

NA ASHA KIGUNDULA-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha wachezaji 24 wa Simba kimendoka nchini jana kwenda Nigeria, kwa ajili ya mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United, utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa New Jos.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ilieleza kuwa, msafara wa timu hiyo ulioondoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Ilieleza kuwa kikosi hicho kitapitia nchini Ethiopia ambapo kilitarajiwa kufika jijini Addis Ababa usiku na kupumzika kwa muda kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Abudja kinakotarajiwa kuwasili leo alasiri.

Katika msafara huo yumo Kocha Mkuu,
Sven Vanderbroeck na msaidizi wake Seleman Matola, wakati wachezaji waliojumuishwa ni John Bocco, Aishi Manula, Ally Salum, Beno Kakolanya, Mohamed Hussein, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Joash Onyango na Gadiel Michael.

Wengine ni Ibrahim Ame, Hassan Dilunga, Francis Kahata, Kennedy Juma na Clatous Chama.

Pia wamo Bernard Morrison, Rally Bwalya, Muzamiru Yassin, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Miraji Juma, Pascal Wawa, Medie Kagere na Luís Miquissone.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles