Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAALAM.
MSANII ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha Wasafi Media, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amezindua rasmi tamasha lake la Wasafi kwa mwaka huu na kulipa jina la ‘Tumewasha’.
Akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini Dar es Salaam, Diamond Platnumz alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litaanzia Mkoa wa Kahama na kufuatiwa mikoa mingine.
“Tunazindua rasmi tamasha letu tour ya Tumewasha na kwa mwaka huu tunaanza na mkoa wa Kahama Jumamosi hii Novemba 28 na baadae mikoa mingine itafuata kutokana na ratiba itakavyokuwa,” alisema Diamond Platnumz.
Kwa sasa msanii huyo anaonekana yupo studio na mkongwe wa muziki kutoka Congo DRC, Koffi Olomide kuandaa wimbo wao.