31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

AZAM VS YANGA: Vita ya wababe

NA ASHA KIGUNDULA-DAR ES SALAAM

SWALI la nani ataibuka mbabe na kuvuna pointi tatu litapatiwa jawabu leo pale timu za Yanga na Azam FC, zitakaposhuka dimbani kuumana, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochewa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaoanza majira ya saa moja usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa vikosi vya timu hizo msimu huu.

Lakini ushindani zaidi utachochewa na nafasi ya timu hizo katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam ikiwa kileleni na pointi 25 sawa na Yanga iliyoko nafasi ya pili kutokana na tofauti ya wastani wa mabao ya kufungana kufungwa.

Timu hizo kila moja imeshuka dimbani mara 11, Azam ikishinda michezo nane, sare moja na kupoteza michezo miwili.

Yanga kwa upande mwingine imeshinda michezo saba na kupoteza michezo minne.

Katika kupachika mabao, Yanga imefunga mabao 13, wakati Azam imepachika mabao 18.

Yanga itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, wakati  Azam itakuwa na maumivu ya kuchapwa bao 1-0 na KMC,Uwanja wa Uhuru.

Rekodi za jumla katika Ligi Kuu za timu hizo zinaonyesha kuwa, Yanga na Azam zimekutana mara 24, kila moja imeshinda 

Timu hizo zilipokutana msimu ulioopita wa Ligi Kuu,mzunguko wa kwanza matokeo yalikuwa suluhu, lakini ziliporudiana mzunguko wa pili Azam ilishinda bao 1-0.

Hata hivyo, safari hii zitakutana Yanga ikiwa na sura mpya katika benchi lake ya ufundi ambalo kwa sasa linaongozwa na kocha Mrundi Cedric Kaze.

Azam haina mabadiliko kwani itaendelea kuongoza na kocha wake Aristica Cioaba ambaye aliikabili Yanga msimu uliopita wakati huo ikifundishwa na raia wa Ubelgiji Luc Eymael kabla hajafungashiwa virago.

Eneo la katikati kwa maana ya viungo ndilo hasa linatarajia kuamua mchezo huo, Yanga ikiwategemea Mukoko Tonombe, Feisal Salum na Carlos Fernandes‘Carlinhos’,.

Azam itakuwa na Salum Abubakar, Richard Jodji na Never Tigere. 

Michezo mingine ya ligi hiyo itakayopigwa leo Ruvu Shooting itaikaribisha Tanzania Prisons na kuumana nayo Uwanja wa Uhuru, Kagera Sugar itakuwa nyumbani dimba la Kaitaba mjini Bukoba kukipiga na  Biashara United ya Mara wakati ambao Mwadui itavuna mashati na Gwambina itakayokuwa ugenini Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles