26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Simba waijia juu Yanga sakata la Okwi

okwiiNA SAADA AKIDA
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, ameibuka na kudai hana muda wa kuumiza kichwa juu ya madai ya klabu yaYanga, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hanspope akiwapa onyo kuwa endapo watafungua kesi wahakikishe wana vielelezo sahihi.

Yanga ilitangaza kumfungulia kesi ya madai ya fidia Okwi, kwa kumtaka ailipe kiasi cha dola 2,100,000 kwa kuvunja mkataba na ada ya mazoezi, huku ikidai kulipeleka suala hilo Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ili liweze kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza na MTANZANIA akiwa visiwani Zanzibar, Okwi alisema hana tatizo na klabu yake hiyo ya zamani hivyo kama wapo tayari kwenda mahakamani ni vyema wakafanya hivyo ili sheria ziweze kufuatwa.

Alisema kwa sasa anataka kutuliza akili yake kufikiria masuala ya soka kwa kushirikiana na wenzake ili kufikia malengo yake na kwamba madai ya Yanga hayamuhusu, kwani amejipanga na tayari ameandaa watu watakaofuatilia suala hilo.

“Kwa sasa akili yangu inawaza mambo ya soka kwani nilikuja Tanzania kucheza mpira hivyo masuala yaYanga hayanihusu, kama wanataka kwenda mahakamani waende ila watambue sheria pekee ndio itatoa haki juu ya hilo,” alisema.

Kwa upande wake Hanspope, aliionya Yanga juu ya uamuzi wao wa kutaka kwenda mahakamani kumshtaki Okwi, huku akiwataka kuhakikisha kuwa na vielelezo vyote.

“Yanga wanatakiwa kuwa makini na jambo hili kwani asilimia kubwa wao ndio wenye matatizo, lakini kama wanataka kwenda mahakamani waende ila wanapaswa kuwa na vielelezo sahihi vinginevyo kesi hiyo itawageukia,” alisema.

Alisema lengo la uongozi wa Yanga ni kutaka kumchanganya kisaikolojia Okwi na kumtoa mchezoni ili ashindwe kuitumikia vyema Simba na kuwatahadharisha endapo wataenda mahakamani, watambue watakutana na majibu kama yaliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumuidhinisha kuichezea klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles