23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa apanda kizimbani

Pg 2Na Mwandishi Wetu, Hai
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amepanda kizimbani na kutoa ushahidi katika kesi utapeli dhidi ya mtu aliyetumia jina la Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta.
Katika kesi hiyo namba 117, Dk. Slaa ni shahidi wa nane na alisema kuwa mke wake, Josephine Mushumbuzi, ndiye aliyemsaidia kumgundua mtu aliyejaribu kumtapeli kwa kutumia jina la Jaji Samatta.
Alikuwa akituoa ushahidi jana katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya Aprili na Mei, mwaka 2012, mshtakiwa Abedi Adamu (24), alitumia jina la Jaji Samatta katika jaribio la kumtapeli Dk. Slaa.
Mshitakiwa huyo anadaiwa alitaka kufanya utapeli huo kwa madai ya kuisaidia Chadema kushinda rufaa aliyoikata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akipinga hukumu ya kumvua ubunge iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Arusha.
Kwa nyakati tofauti, mshitakiwa huyo (Abeid) alijitambulisha kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalla Safari, Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kuwa yeye ni Jaji Samatta akiwataka wampe fedha awasaidie kushinda rufaa hiyo.
Akiongozwa na Waendesha mashitaka, Mawakili wa Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Susan Kimaro na Furahini Kibanga, Dk. Slaa alisema baada ya kuona anaendelea kupata shaka juu ya mtu alimueleza mke wake kwa (Josephine) kwa kuwa ni mtaalamu wa mawasiliano (IT) ambaye alifanya kazi ya kumtambua mtuhumiwa huyo aliyekuwa anajiita ni Jaji Samatta.
“Baada ya kuona naendelea kupata shaka na mtu huyu, niliwasiliana na Jaji mstaafu, Thomas Mihayo, nikamwomba kupata namba za Jaji Samatta, nikampigia Lema na Profesa Safari.
“Lakini kwa kuwa mke wangu ni mtu wa IT, nilimpa kazi ya kumtambua huyu mtu… alimtumia Sh 500 kwa njia ya M-PESA na baadaye akanitumia ujumbe kuwa namba (0754013237) za huyo anayejiita ni Jaji Samatta zimesajiliwa kwa jina la Abeid Abeid,” alisema Dk. Slaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles