29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Simba waichokoza tena Yanga

img_2428

Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Simba, imewataka watani wao wa jadi, Yanga, wasubiri mzunguko wa pili waone moto watakaouwasha na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Ligi Kuu mzunguko wa kwanza imemalizika Alhamisi iliyopita, huku Simba wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 35, Yanga wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 33.

Kutokana na tofauti ya pointi mbili walizopishana na Yanga, Simba wamewaambia Yanga kuwa huu ni msimu wao, hata kama wamewakaribia, bado wao wapo kileleni mwa ligi hiyo na kwamba hata mzunguko wa pili hawatawapita.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Meneja wa timu ya Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema maneno ya wapinzani wao hayawezi kuwakatisha tamaa na badala yake wasubiri mzunguko wa pili uanze ili waone malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

“Hayo ni maneno ya kawaida ambayo hayawezi kutukatisha tama, kwani tayari tumeshawapita kwa pointi mbili ambazo wao wanaziona ndogo.

“Kwa sasa hawawezi kufanya lolote kutukuta au kutupita, hadi mzunguko wa kwanza umemalizika kwa mechi 15 tulizocheza, wasuburi mzunguko wa pili uanze ndio tutajua nani amefanikiwa kutimiza lengo lake la kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mgosi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles