30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Nimonia inaua watoto Afrika

rtpneukidmark

NEW YORK, MAREKANI

ASILIMIA 60 ya vifo milioni 5.9 vya watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 5 vilivyotokea mwaka jana katika nchi za Afrika na Asia vilitokana na ugonjwa wa kichomi au nimonia.

Utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na ripoti yake kuchapishwa jana katika jarida la kimataifa la masuala ya afya la Lancet Medical Journal, umebainisha kuwa, ugonjwa huo ndio unaosababisha vifo vingi kwa watoto wadogo katika nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola, Ethiopia na Nigeria.

Aidha, ripoti hiyo imesema kuwa, licha ya kuwepo chanjo ya ugonjwa huo, lakini katika kila watoto 1,000 walio na chini ya miaka mitano, 90 hufariki dunia kutokana na nimonia katika nchi za Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Mali, Nigeria, Sierra Leone na Somalia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles