24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Msuva: Wanaonifananisha na Kichuya wanakosea

kichuya-msuva

Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

WINGA machachari wa timu ya Yanga, Simon Msuva, amesema wale wote wanaomfananisha na mshambuliaji wa timu ya Simba, Shiza Kichuya, wanakosea.

Msuva amesema hayo alipokuwa akizungumza na MTANZANIA Jumapili, baada ya kuwepo mvutano kwa wadau wa soka juu ya yeye na Kichuya nani zaidi uwanjani.

Msuva amesema anafanana na Kichuya kwa kuwa wote ni binadamu na wana jnsia inayofanana, lakini ukija  kwenye ubora uwanjani wana tofauti kubwa, huku akijinasibu kumzidi mwenzake.

Alisema kuanza kuangalia kati yao nani mzoefu wa ligi lazima jibu litakuja kuwa yeye na hata msimu huu ukiangalia pasi za mwisho za mabao kati yao, aliyeisaidia zaidi timu yake bado kura zitamuangukia.

“Sijaona tunachofanana mimi na Kichuya kisoka, kwani nimepata tuzo ya ufungaji na mchezaji bora wa msimu ambapo yeye hajaipata, pia mimi ni mzoefu kwenye ligi zaidi yake.

“Tukija msimu huu katika ligi, sawa anaongoza  kwa ufungaji kwa mabao tisa, mimi nikiwa na saba, lakini nimempita kwenye kutengeneza mabao, kwani nimetengeneza 14, Kichuya ametengeneza nafasi nne tu, hivyo ni tofauti kubwa, ila yote kwa yote tusubiri ligi ifike mwisho tutajua nani ni nani,” alisema Msuva.

Wachezaji hao kwenye Ligi Kuu msimu huu wametwaa tuzo ya uchezaji  bora wa  mwezi, Kichuya akichukua ya Septemba, huku Msuva akitwaa ya Oktoba, lakini wakijikuta wakiingia pamoja kwenye kinyang’anyiro hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles