Theresia GaspeR-Dar es Salaam
MICHUANO ya Kombe la Shirikisho(ASFC)hatua ya 32 bora, inatarajia kuendelea leo, ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa Mwadui, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba iliingia hatua hiyo, baada ya kuifunga Arusha FC mabao 6-0, kwenye dimba hilo, wakati Mwadui iliitimua mashindanoni Mkamba Rangers, kwa kuichapa mabao 4-1, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Simba na Mwadui zilipokutana mara ya mwisho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu uliopigwa Uwanja wa Kambarege, Shinyanga.
Katika mchezo huo, Mwadui ilishinda bao 1-0.
Simba itashuka dimbani ikitoka kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo, ikiipiga mabao 2-1 Mbao kabla ya kuitungua Alliance mabao 4-1. Michezo yote ikipigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Hii ina maana Simba itataka kulipa kisasi huku Mwadui ikikusudia kuendeleza wimbi la ushindi ingawa itaingia uwanjani na jeraha la kupigwa bao 1-0 na Azam katika mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Kambarage.
Michezo mingine ya ligi hiyo leo, JKT Tanzania itaikaribisha Tukuyu Stars, mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru, Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani Uwanja wa Gairo kupepetana na Sahare All Star ya Tanga, Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Mighity Elephant, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Ndanda,
itakuwa dimbani kuumana na Dodoma Jiji, Uwanja wa Gwambina Complex,
Mwanza, Ruvu Shooting itakuwa mgeni wa
Gwambina.
Afrinas Sports itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuumana na Alliance, wakati ambao Ihefu ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Gipco, Uwanja wa Ihefu.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema wamejiandaa kiushindani kwani wanahitahitaji kupata ushindi na kusonga mbele zaidi.
“Tunakutana na Mwadui, timu ambayo ni nzuri. Mara ya mwisho tulipokutana walitufunga hivyo lazima tuwe makini tusifanye makosa ili tupate pointi tatu muhimu,” alisema.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Mwadui, Khalid Adam, alisema wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi mbele ya Simba, hivyo watapambana kukamilisha lengo.
“Wachezaji wote wapo salama wamejiandaa kwa ajili ya mchezo, nafahamu utakuwa na ushindani mkubwa ila tumejipanga vizuri,” alisema.