24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Kourtney akanusha kuwa mjamzito

Los Angeles, Marekani

DADA wa Kim Kardashian, Kourtney, amekanusha kuwa na ujauzito baada ya wiki moja iliyopita kuposti picha iliyowaacha vinywa wazi mashabiki.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 40, aliposti picha inayomwonyesha akiwa na tumbo kubwa tofauti na ilivyozoeleka.

“Hakuna ukweli wowote juu ya ujauzito japo natamani kuongeza familia hapo baadaye lakini kwa sasa huu ni mwonekano wangu wa sasa na wala sina ujauzito,” alisema mrembo huyo.

Kourtney  anayedaiwa kurudiana na mpenzi wake wa zamani Younes Bendjima ni mama wa watoto watatu ambao ni Mason mwenye miaka 10, Penelope miaka saba na Reign mwenye miaka mitano.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles