22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kurudisha heshima kambi ya Zanzibar

simba_sc-600x400NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amesema kuwa kambi ya Zanzibar itakuwa nzuri kwenye michezo yake mitano ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosalia.

Simba imeondoka Dar es Salaam jana kwenda Unguja kuweka kambi ya siku nne kabla ya kuwakabili Azam FC kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Aprili 30 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mayanja alisema mechi ya Azam anaipa umuhimu mkubwa lakini pia mipango yake ni kuhakikisha anashinda michezo yote iliyobaki ya ligi.

“Nina matumaini makubwa na chaguo langu la kambi ya Zanzibar hasa baada ya kupita upepo mbaya katika kikosi changu, lakini pia kurejea kwa kiungo wangu, Mwinyi Kazimoto, aliyekuwa majeruhi ni faraja nyingine inayoniaminisha tutakaporejea  timu itakuwa mpya,” alisema Mayanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles