23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Coastal Union yasaka manoti kwa Yanga

Kikosi-cha-Coastal-Union-01NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Coastal Union ya Tanga, umeahidi kuwazawadia fedha wachezaji wake iwapo itaifunga Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Inadaiwa wachezaji wa timu hiyo wameahidiwa donge nono iwapo wataifunga Yanga katika mchezo huo ambapo bingwa ataiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Coastal Union imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Simba kwenye hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Yanga wao wameingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Habari ambazo MTANZANIA Jumamosi limezipata kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa wachezaji wa Coastal Union wameahidiwa Sh 200,000 kila mmoja kutoka kwa wadau mbalimbali wa mkoa huo iwapo wataiondosha Yanga kwenye hatua hiyo.

“Hivi sasa suala la ligi tumeliweka pembeni kwani tayari tuna uhakika wa kubaki katika ligi msimu ujao kulingana na mipango iliyopo, hivyo tunaelekeza nguvu zetu FA ili angalau nasi tupate nafasi ya kuiwakilisha nchi.

MTANZANIA lilipomtafuta Meneja wa timu hiyo, Razack Yusuph, alisema kuwa  hivi karibuni kumekuwa na wadau wengi ambao wamejitokeza kuisaidia timu yao katika mechi zake za ligi na za FA lakini hawezi kusema kama fedha zinazotajwa kutolewa kwa wachezaji baada ya kuifunga Yanga zipo au hazipo.

“Unajua hivi karibuni tumekuwa tukipata sapoti kubwa kutoka kwa wadau wa soka hapa Tanga na hiyo yote kuhakikisha timu inasalia kwenye ligi na hata kupata nafasi ya ushiriki wa FA mwakani, hivyo hilo jambo linaweza kuwepo au lisiwepo lakini kikubwa tunahitaji matokeo ya ushindi dhidi ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles