26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Simba hesabu zagoma

 ONESMO KAPINGA 

MPANGO wa benchi la ufundi la Simba kushinda michezo mitano mfululizo ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, umeingia dosari baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Wekundu hao baada ya sare ya jana wamefikisha pointi 72, baada kushuka dimbani mara 29, wakishinda 23, sare tatu na kupoteza tatu, lakini wakisalia katika uongozi wa ligi hiyo. 

Kama wangefanikiwa kupata ushindi katika michezo mitano mfululizo ukiwemo wa jana, wangefikisha pointi 86 na kutwaa ubingwa kwani hakuna timu nyingine inayoweza kufikisha pointi hizo hata kama itashinda michezo yake yote iliyosalia. 

Washindani wa karibu katika taji la ligi hiyo ni Azam ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 54 kabla ya mchezo wake wa jana dhidi ya Mbao FC na Yanga yenye pointi 54 ,lakini ikishika nafasi ya tatu kutokana na kigezo cha wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. 

Yanga na Azam kama zitashinda michezo yao yote iliyosaliwa zitafikisha pointi 84. 

Mchezo wa jana uliochezeshwa na mwamuzi Abdallah Mwinyi Mkuu kutokaSingida, Simba ioiandika bao la kuongoza dakika ya 11 kupitia kwa Shiza Kichuya, baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa Shooting, Mohamed Makaka. 

Kabla ya kufunga, Kichuya alipiga shuti kali lililotemwa na kipa huyo na mpira kumrudia tena na kufunga kirahisi. 

Shooting ilifanya shambulizi zuri dakika ya 13, lakini mabeki wa Simba wakiongozwana Pascal Wawa, walikuwa imara kuondoa hatari langoni kwao 

Simba ilitengeneza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 22, baada ya Gadiel Michael kupanda mbele kusaidia mashambulizi na kupiga shuti ambalo halikulenga lango. 

Dakika moja baadaye, Simba ilifanya shambulizi jingine kwa shooting lakini Hassan Dilunga alishindwa kufunga baada ya shuti lake kutokana nje. 

 Hata hivyo, Shooting ilishindwa kufunga dakika ya 31, baada ya Graham Naftal kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa Simba, Aishi Manula. 

Shooting ilisawazisha bao dakika ya 36 lililofungwa kwa kichwa na Fully Maganga, akiunganisha kona iliyopigwa na Abdallahman Musa.

Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa na nguvu sawa baada ya kufungana 1-1.

Simba almanusura ipate bao dakika ya 52, baada ya Meddie Kagere kupiga shuti lililodakw na Makaka.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbloeck alifanya mabadiliko dakika ya 59, alimtoa Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Francis Kahata kabla ya kumwingiza Deo Kanda dakika 67 kuchukua nafasi ya Dilunga na kisha kumtoa Gadiel na kumwingiza Mohamed Hussein.

Shooting nayo ilifanya mabadiliko, walitoka Maganga na William Patrick na nafasi zao kuchukuliwa na Jamal Mnyate na Sadat Mohamed dakika ya 68.

Pamoja na mabadiliko yaliyofanywa kila upande, dakika 90 za kipute hicho zilikamilika kwa sare ya bao 1-1.

Naye Ofisa wa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire aliwapongeza vijana kwa kuonyesha mchezo mzuri kwa akili na kwa tahadhari.

Bwire alisema lengo lao lilikuwa kuwaonyesha Simba wadogo kiushindani bali wakongwe tu katika soka.

“Vijana wamjituma kwa nguvu na wameeonyesha viwango vya hali ya juu, wazee wamechoka licha ya kupata bao moja kwa bahati sana,” alisema Bwire.

Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Luis Miquissone, Meddie Kagere, John Bocco na Shiza Ramadhan.

Ruvu Shooting: Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Rajab Zahir, Baraka Mtuwi, Abdallahman Musa, Shaban Msala, Graham Naftal, Fully Maganga na William Patrick.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles