24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kura za maoni ‘zamtupa Trump’

 WASHINGTON, MAREKANI

KURA kadhaa za maoni zinaonyesha Rais wa Marekani, Donarld Trump yupo nyuma ya mgombea urais wa Democrat, Joe Biden kwa wigo mpana.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Novemba, mwaka huu. Kuna ripoti kambi ya kampeni ya Rais Trump imeandamwa na migogoro na urais wake umekumbwa na janga baada ya janga.

Rais Trump ni mwanasiasa asiyetabirika. Miaka minne iliyopita aliingia kikaangoni na kuonekana kutofaa – lakini akaweza kupindua matarajio ya wengi akashinda tiketi ya urais kwa chama chake na kushinda uchaguzi mkuu.

Safari ya namna hiyo, kama inavyotarajiwa, inampa mtu kujiamini zaidi katika maamuzi.

Katika hali ya kawaida, ni rahisi kuona namna ambavyo Trump alipata ushindi miaka minne iliyopita baada ya kupita kwenye tanuri la kashfa na magomvi na kudhani kuwa atafanya hivyo pia mwaka huu.

Wataalamu walikosea miaka minne kwenye tathmini zao. Trump alikea sahihi.

Rais Trump alikuwa sahihi katika baadhi ya mambo. Aliingia ulingoni akiwa mgeni wa siasa katika kipindi ambacho raia wengi walikuwa wamechoshwa na mfumo wa siasa za nchi hiyo. Akatumia mwanya huo ipasavyo kushinda uchaguzi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles