23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Makonda awaomba viongozi wa dini kuombea Watanzania

Brighiter Masaki

Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuombea Watanzania, kufunguliwa fahamu zao maana wengi wao wamefugwa kifikra.


Alisema Maaskofu na Mashekh tuombe Mungu ili tusaidie Watanzania waweze kufunguka kifikra na fahamu zao wajuwe kuwa Tanzania ni nchi tajiri, wengi wamefungwa pasipo kujijuwa.


Akizungumza wakati wa mkutano wa maridhiano wa viongozi wa dini, ambao wapo kwenye kamati ya kusimamia Ulinzi na Usalama, jana jijini humo Makonda alisema kuwa maridhiano yanaanza kwa ngazi ya familia na wanatakiwa kuombeana wao kwa wao.


“Watanzania wakifunguliwa fahamu zao kutakuwa na maridhiano katika ngazi ya familia, wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla.


“Wamekuja watu wengi maskini lakini sasa hivi wananufaika na kufanikiwa na mkoa wetu wakati wenye mkoa hawanufaiki, na kitu chochote na watu wanatakiwa wafunguliwe fahamu zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambae pia ni Shekh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum amesema mbali na kumpongeza Rais kwa kusimama imara kuhakikisha makanisa na Misikiti havifungwi pia wanaunga mkono kwa asilimia mia moja juhudi anazofanya katika kuliletea Taifa Maendeleo.


Katika Kikao hicho Sheikh Mussa amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda kwa namna anavyoendesha Mkoa huo jambo linalofanya hali ya amani na utulivu kuendelea. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles