26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

‘Sijazoea’ yamliza mke wa AT

ATNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MWIMBAJI wa muziki wa mduara, Ally Ramadhani ‘AT’, amesema ameshangazwa kwa mara ya kwanza kumuona mkewe akitoa macho baada ya kusikia wimbo wake mpya wa ‘Sijazoea’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, AT alisema, mkewe amekuwa hana kawaida ya kusikiliza nyimbo zake, lakini ameshangazwa kumuona akiusikiliza wimbo huo na kulia.

“Kitendo hicho kimenifurahisha sana na nimejiona nimefanya kazi nzuri, mke wangu yupo tofauti, hapendi na wala hatakagi kusikiliza kazi zangu, lakini kwa mara ya kwanza nimemkuta akiusikiliza wimbo huu,” alisema AT.

Alisema, wimbo huo ameuachia siku tatu zilizopita na umekuwa ukipigwa sana Zanzibar na tayari umeanza kuvuta hisia za mashabiki wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles