Dimpoz kutambulisha mpya Marekani

0
1531

ommyNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anatarajia kuanza kutambulisha nyimbo mpya katika ziara yake nchini Marekani, Februari 13 hadi 15, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ommy Dimpoz alisema ziara hiyo itakuwa ya kwanza tangu mwaka huu ulipoanza.

“Natarajia kuanza ziara yangu ya kwanza tangu mwaka huu umeanza, nilikwenda Kenya na kufanya kazi moja na Avirl kisha nikarudi nyumbani,” alisema Ommy Dimpoz.

Alisema mbali na kufanya ziara hiyo ya siku tatu, atarejea nchini na kuondoka tena, kwani ratiba yake inaonyesha Februari 21 atakuwa na shoo maalumu jijini New York.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here