27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Barcelona kuivaaTanzania All StarsMachi 28

Pg 32NA MWANDISHI WETU

TIMU ya wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona,wanatarajia kuvaana na magwiji wa Tanzania,‘Tanzania All Stars’kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 28, mwaka huu.

Ujio huo mkubwa ni wa pili kutokea nchini ndani ya miezi sita iliyopita, ambapo Agosti mwaka jana magwiji wa Real Madrid walitua nchini na kucheza na magwiji wa hapa, mchezo ulioisha kwa Madrid kushinda mabao 3-0.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwakilishi wa wachezaji hao wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert, alisema mechi hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka tofauti.

“Kikosi chetu kina wachezaji nyota ambao ni maarufu duniani na naamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa,” alisema.

Kluivert alisema yeye ni mwenyeji sana Tanzania, kwani huu ni ujio wake wa tatu nchini na anaamini kuwa jinsi mashabiki wa soka wanavyopenda sana soka, itakuwa ni fursa kubwa kwao kuona vipaji vya zamani vilivyotukuka.

“Ninafurahi kuja nchini Tanzania kwa mara ya tatu, ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini kwa mara ya kwanza, naomba mashabiki wa soka wajae uwanjani kwa wingi kuona mpira wenye ushindani,” alisema Kluivert.

Naye mwakilishi wa Kampuni ya Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo nchini, Stuart Kambona, alisema madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha uhusiano wa kibiashara wa mpira wa miguu baina ya Tanzania na Hispania, kutangaza utalii na kuendeleza uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Kambona alisema pamoja na mchezo huo siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza Tanzania nje ya mipaka yake na kuleta fursa nyingi hapa nchini.

“Wachezaji wa Barcelona wataingia nchini siku mbili kabla ya mechi na watakuwa zaidi ya 20, majina ya wachezaji wengine yatatangazwa baadaye, ila tunaomba wadhamini wajitokeze kufanikisha na kufaidika na mechi hiyo,” alisema Kambona.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo, aliwaomba mashabiki wa soka kujiandaa kuangalia mechi hiyo, huku akiwataka kufika kwa wingi uwanjani siku hiyo.

Kasongo alisema DRFA imefarijika sana kwa ziara hiyo na kuiomba Prime Time Promotion kuhakikisha kuwa inapanua wigo kwa kuandaa mechi nyingi ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo ya soka nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles