27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SIGARA HUUA MILIONI SABA KILA MWAKA

Na  VERONICA ROMWALD-ALIYEKUWA KENYA


WATU milioni saba hufariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku hususan uvutaji sigara, imeelezwa.

Takwimu hizo ni matokeo ya utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki iliyopita Nairobi, Kenya katika warsha ya siku ya mbili ya kukabiliana na matumizi ya Tumbaku.

Kwa mujibu wa WHO idadi ya wavutaji wa sigara huenda ikaongezeka hadi kufikia bilioni moja ifikapo 2025.

WHO linaonya kuwa iwapo juhudi za kuelimisha jamii juu ya athari zitokanazo na bidhaa hizo hazitachukuliwa idadi ya vifo itaongezeka.

Wadau wa sekta ya tumbaku walikutana hivi karibuni nchini Kenya kujadiliana namna ya kukabiliana na matumizi ya tumbaku kwa kutumia njia ya teknolojia.

Katika warsha hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na Kampuni ya Oxygene, iliyopewa kauli mbiu isemayo ‘kupunguza madhara ya tumbaku, kuelekea dunia isiyo na wavutaji,’ waandishi wa habari zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika walihudhuria.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Malawi, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Zambia, Botswana, Swaziland, Lesotho, Ethiopia, Nigeria, Mozambique na Afrika Kusini.

Akiwasilisha mada katika warsha hiyo, Mshauri wa Vyombo vya Habari wa WHO, Magesha Ngwiri alisema takwimu zinaonyesha Bara la Afrika lina kiwango kikubwa cha wavutaji kuliko mabara mengine.

“Linachangia kwa kiwango cha asilimia 80, matokeo ya utafiti wa WHO ya mwaka 2010/11 yanaonyesha vijana wenye umri kati ya miaka 13 na 15 barani humu walibainika wameanza kuvuta sigara,”  alisema.

Aliwataka waandishi kufanya utafiti wa kina kubainisha kiwango cha uvutaji kilichopo.

“Lengo ni kuielimisha jamii na kuziamsha Serikali kuanza kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo,” alisema.

Rais wa Shirika lisilo la kiserikali la Leadership Impact Dynamics, Ade Adeyami alisema iwapo hatua hazitachukuliwa itakuwa vigumu kwa Bara la Afrika kufanikisha lengo la tatu la Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).

“Linahimiza afya bora kwa wote, takwimu zinaonyesha kiwango cha matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku duniani ni kikubwa kulinganisha na mabara mengine, lazima tuchukue hatua,”  alisema.

Mhadhili na mwanachama wa kudumu wa Taasisi ya Biashara ya Gordon, Chuo Kikuu cha Pretoria, Dk. Tendai Kadenhe Mhizha, alisema takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) zilizotolewa mwaka 2012 zinaonyesha matumizi ya tumbaku yalisababisha vifo vya watu takriban milioni 38 duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles