26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA: NI UCHAGUZI WA KIKATILI, TUMEJITOA…

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema macho yao sasa wameeelekeza katika kata 38 zilizobaki baada ya kujitoa kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani katika kata tano za Jimbo la Arumeru Mashariki kwa madai ya ukatili na mashambulizi wanayofanyiwa baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho.

Aidha, amewataka vijana wa chama hicho kujitetea wanaposhambuliwa na polisi na wasisubiri tamko la chama ambapo pia katika mkutano wake na waandishi wa habari wilayani Arumeru, ametaja Kata zilizojitoa kuwa ni Ngabobo, Leguruki, Makiba, Maroroni na Mbureni.

“Nimewasiliana na Mkurugenzi wa Uchaguzi, bwana Kailima ameniambia yuko Tunduru, mambo haya viwango vinatofautiana katika hatua ya sasa tumejitoa katika kata tano hizi na tutaendelea kuangalia katika kata nyingine 38 zilizobaki lakini tunafuatilia kwa karibu matukio haya.

“Kuna matukio mengi ya polisi kuumiza watu na sisi tunachelea kuruhusu vijana wetu kutoka kupiga watu kwa sababu hatuna sababu ya kupiga raia wetu wanapokwenda kutekeleza wajibu wao.

“Lakini tunapenda kuwaambia vijana wetu popote walipo wasikunje uso wanapoendelea kupigwa au wanapofanyiwa mashambulizi basi wajitetee, watafute utaratibu wa kujitetea wasisubiri tamko la chama wajitetee kunusuru maisha yao,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema mambo hayo yana mwisho wa uvumilivu wake kwani wanaona vyombo vya dola vinavyotumika vibaya huku polisi wakishuhudia.

“Kamanda Mkumbo (Charles Mkumbo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa arusha) anajua yote haya, kama hajui hastahili kuwa ofisini lakini vijana wake ndiyo wanaongoza vijana wa ‘green guard’ wanapiga watu wanaumiza, wanakata mapanga, wanateka watu wanateka vuongozi.

“Arumeru hakuna uchaguzi kuna upumbavu na upuuzi ni fujo tu na zimasimamiwa na vyombo vya dola. Sisi kwa hali hii inayoendelea Arumeru tunawaagiza viongozi wetu wa chama na madiwani wetu haraka sana wajitoe, mawakala wetu ambao wamekuja vituoni mchana huu waondoke wote waachanae na uchaguzi huu wa kikatili tuwaachie wao waendelee na viongozi wote Chadema wasiende kwenye majumuisho ya kura hizi ambazo haziakisi maamuzi ya wanachi ama utashi wa wananchi,” amesema Mbowe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles