26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Shuka, blanketi marufuku misibani wilayani Rungwe

Striped Wool Blankets

Na Ibrahim Yassin, RUNGWE

SERIKALI Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, imepiga marufuku watu kutoa msaada wa shuka na blanketi katika misiba ili kuepusha ugomvi kwa wanandugu baada ya msiba kumalizika.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja baada ya kutokea ugomvi wa mara kwa mara kwa ndugu kugombea vitu hivyo vinavyopelekwa misibani wanapofiwa na kuleta uhasama katika koo mbalimbali.

Aidha, badala ya kuendeleza mila hiyo ambayo inadaiwa imepitwa na wakati wametakiwa kupeleka   vyakula ili viwasaidie wakati wa msiba.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ibungu, Daniel Mwakalinga, alisema kuna baadhi ya familia   zimekuwa na uhaba wa chakula na kulazimika  kuuagiza uongozi wa Serikali za vitongoji  kutoa fedha, huku wananchi wakipeleka nguo, mablanketi  na mashuka kuwahani wafiwa.

“Wananchi wanatakiwa watii agizo hilo ili kuepusha migogoro inayoepukika, kinyume na hivyo sheria itachukua mkondo wake ikiwamo kutozwa faini  kwa yeyote atakayebainika kuendeleza mila hizo,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikubo, Edward Mwaisango, alisema kuendekezwa mila za  kupeleka vitu hivyo misibani hakuna tija badala yake walengwa hao wasaidiwe wanapokuwa hai.

“Wananchi wanapaswa kupeleka vyakula kama  sukari, mahindi, mchele na fedha ambapo kwa  kufanya hivyo kunaweza kusaidia wafiwa wakati wa msiba,” alisema.

Kutokana na agizo hilo, baadhi ya wananchi wamejikuta katika wakati mgumu wa kushindwa kutekeleza mila hiyo na wametaka jamii ielimishwe misaada ya kuchangia kabla ya misiba kutokea.

“Ni jambo zuri Serikali kukataza vitendo hivyo, lakini pia jamii ielimishwe kutoa misaada ya matibabu kwa wagonjwa kabla hawajafariki badala ya kupeleka vitu hivyo pindi mgonjwa anapofariki,” alisema mmoja wa wakazi hao, Elias Asajile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles